Umoja wa Bodaboda
Jiji la Arusha

Bodaboda usafiri salama · bodaboda kazi kama kazi nyingine

9,913 Wanachama
683 Vituo
25 Kata jijini Arusha

Utangulizi

Chama hiki si cha Kiserikali, Kisiasa, kabila wala cha Kidini. Kitatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia masharti na madhumuni yaliyoainishwa ndani ya Katiba ya chama, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na sheria nyingine za nchi.

Dira, dhima na kauli mbiu

Dira

Kuwa chombo imara cha kutetea haki za madereva wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu ambao ni wamiliki kibiashara, na kuhamasisha na kutetea haki za abiria.

Dhima

Kuwaunganisha wanachama katika kuweka mazingira bora ya biashara, kutetea haki na maslahi yao, na kuhakikisha wanapata elimu katika tasnia ya usafirishaji abiria.

Kauli mbiu

Bodaboda usafiri salama.
Bodaboda kazi kama kazi nyingine — usichukulie poa.

Lugha rasmi

Lugha rasmi katika shughuli za chama ni Kiswahili na Kiingereza.

Madhumuni makuu ya umoja

  1. Kulinda haki, wajibu na maslahi ya dereva na mmiliki ambaye ni dereva.
  2. Kusimamia, kuendeleza na kulinda maslahi ya watumiaji wa pikipiki ndani ya wilaya katika mamlaka za Serikali na Umma, ili kuwe na mazingira mazuri ya biashara ya usafirishaji abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu.
  3. Kuhakikisha madereva wote wa pikipiki za abiria kibiashara wanafuata sheria za usalama barabarani.
  4. Kuwa mdau mkubwa wa usalama barabarani, kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara ili ajali zipungue.
  5. Kuwakutanisha madereva na wamiliki kujadili maendeleo na changamoto zao, na kutafuta mbinu za kuzitatua kwa kushirikiana na wasimamizi wa sheria.
  6. Kujadili na kushauriana na wakuu wa mamlaka zinazosimamia kanuni na sheria za matumizi ya barabara, kwa niaba ya wanachama.
  7. Kuishauri Serikali kuhusu maendeleo ya huduma ya usafiri wa pikipiki, kama utaratibu wa maegesho na uongozi katika maegesho.
  8. Kusaidiana katika shida zilizo ndani ya uwezo wa wanaumoja: ugonjwa wa mwanachama, mke na watoto wanne; msiba wa mwanachama, baba, mama, mke na watoto wanne; kusaidia watoto yatima na wasiojiweza; kutembelea wagonjwa hospitalini na kuchangia damu.
  9. Kudumisha amani, umoja na mshikamano, kuomba tenda jijini Arusha, na kuanzisha taasisi ya mikopo ya pikipiki, vipuri, fedha, viwanja na nyumba kwa wanaumoja.

Jinsi ya kutupata

Wewe ni mwanachama au kiongozi?

Ingia kwenye mfumo kuona taarifa zako na za kituo chako.

Ingia